sw Swahili en English

Huduma zinazotolewa na Kikundi cha WYT

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Juma tatu, 10 Mwezi wa 2, 2020 18:16
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 1984

Kikundi cha WYT kimejikita katika kufanya shughuli mbalimbali na kutoa huduma kwa wanakikundi na wanajamii. Kazi na huduma zinazofanywa na kikundi hiki ni pamoja na:-

  • Ununuzi wa Hisa (Uwekezaji katika Hisa): Kikundi cha WYT kinauza Hisa kwa wanachama wa kikundi tu. Hisa hizi zinalenga kuongeza mtaji wa kikundi na akiba ya mwanachama. Hisa zinazouzwa na kikundi zimegawanyika katika makundi mawili; Kundi la Kwanza ni Hisa za Kawaida, Hizi ni Hisa ambazo ni lazima kwa kila mwanakikundi kununua kila mwezi ili awe na sifa ya kuwa mwanachama hai wa kikundi hiki. Hisa Moja inauzwa Tshs. 10,000 na mwanakikundi anaruhusiwa kununua Hisa zisizopungua 5 na zisizozidi 15 kwa mwezi. Kundi la Pili ni Hisa za Mkupuo, Hizi ni Hisa zinazouzwa na kikundi kwa msimu kwa lengo la kuongeza mtaji wa kikundi na zinauzwa kulingana na mahitaji yaliyopo.
  • Akiba ya Hiari: Hii ni akiba ambayo mwanakikundi anaiweka kwa hiari yake mwenyewe kwa kipindi maalum. Kikundi kinatoa riba kwa mwanakikundi anayewekeza fedha zake kupitia Akiba ya Hiari kulingana na kiwango cha akiba kilichowekezwa na muda wa akiba uliyowekwa.
  • Huduma za Mikopo: Kikundi kinatoa huduma za mikopo kwa wanakikundi wa WYT tu kwa riba nafuu. Mikopo hii imegawanyika kwenye maeneo makuu 3 ambayo ni Mikopo ya Kawaida, Mikopo ya Dharura na Mikopo ya Viwanja/Mashamba. Mikopo ya viwanja na mashamba pamoja na mikopo ya Dharura ni mikopo inayotolewa kwa wanakikundi wote kwa kuzingatia vigezo na masharti na mikopo hii haina riba yoyote. Mikopo ya kawaida inatolewa kulingana na idadi ya Hisa anazomiliki mwanakikundi ndani ya kikundi (Hadi mara 3 ya Hisa zake), lakini mwanakikundi haruhusiwi kukopa zaidi ya 25% ya mtaji wa kikundi na kwasasa ukomo anaoruhusiwa mwanakikundi kukopa si zaidi za Tshs. 50,000,000.
  • Kufanya shughuli za uwekezaji (IGAs): Kikundi pia kinashughulika na shughuli za uwekezaji na uendeshaji wa Biashara kwa lengo la kutengeneza faida na kuongeza mtaji wa kikundi. Biashara au uwekezaji unaofanywa na kikundi unategemea na hali ya masoko na uwezo wa kikundi kwa kipindi husika.
  • Kuendesha mafunzo mbalimbali ya ubunifu na uendeshaji wa miradi: Kikundi pia kinatoa mafunzo mbalimbali ya ubunifu na uendeshaji wa miradi. Mafunzo haya yanatolewa na wanakikundi wenye uzoefu katika uendeshaji wa shughuli za miradi ya kijamii na kikanisa.
  • Kutoa ushauri elekezi kwa masuala mbalimbali ya kimaendeleo. Kikundi kinatoa huduma za ushauri elekezi (Consultancy Services) katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na usimamizi na uendeshaji wa kikundi.