sw Swahili en English

Malengo na Madhumuni ya kuanzishwa kwa Kikundi cha WYT

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Juma tatu, 10 Mwezi wa 2, 2020 18:15
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 4464

Kikundi cha WYT kiliundwa kikiwa na malengo makuu 2 ambayo ni:-

  1. Kuboresha maisha ya wanakikundi kwa kuwawezesha kuweka akiba na kukopa, kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa juhudi na maarifa.
  2. Kushiriki masuala ya kijamii na kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii

Pamoja na malengo hayo kikundi hiki pia kilikuwa na madhumuni yake yaliyokuwa yanalenga kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii kwa wanakikundi na jamii kwa ujumla. Madhumuni ya kuanzishwa kwa kikundi hiki yalikuwa ni: -

  1. Kuboresha hali ya kiuchumi kwa wanakikundi ili kufikia malengo yao
  2. Kubuni, Kuanzisha na kuendeleza vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya wanakikundi.
  3. Kubadilishana mawazo, Kufahamiana na kusaidiana katika hali mbalimbali za kimaisha.
  4. Kuimarisha Umoja na mahusiano kwa wanakikundi na kuwa na wakati wa pamoja kama Retreat na family get together.
  5. Kushirikiana, kufarijiana na kusadiana katika dhiki na faraja.
  6. Kuendesha na kuwa na ziara za mafunzo kwa wanakikundi.