sw Swahili en English

Uongoziwa Kikundi

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Juma nne, 03 Mwezi wa 3, 2020 06:58
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 1638

Mfumo wa uongozi katika kikundi cha WYT umegawanyika katika maeneo makuu 3; Mfumo wa kwanza ni Kamati tendaji (KT), Mfumo wa Pili ni Sekretarieti ya Uongozi (SU) na Mfumo wa Tatu ni CELL za Kikundi (CK). Msemaji mkuu wa kikundi ni Mwenyekiti wa Kikundi.

Shughuli za siku kwa siku za kikundi zinafanywa na kamati tendaji; Sekretarieti ya Uongozi inashughulika na masuala ya mipango, uwekezaji na usimamizi wa mikopo ya kikundi. CELL za kikundi ni ngazi ya chini ya mfumo wa uongozi wa kikundi cha WYT lakini chenye maamuzi ya kusajili wanakikundi pamoja na kupitisha na kusimamia mikopo ya wanakikundi katika ngazi ya CELL.

Pamoja na mifumo ya uongozi katika kikundi hiki cha WYT, Mkutano mkuu wa wanakikundi wote (AGM) ndicho chombo chenye maamuzi ya mwisho juu ya mambo yote ya kikundi na mipango yote ya kikundi inapitishwa na Mkutano mkuu wa kikundi unaofanyika mara moja kwa mwaka.

Uchaguzi wa viongozi wa kikundi katika ngazi zote hufanyika kila mwaka na kiongozi anaweza kuchaguliwa kwenye nafasi husika kwa miaka 2. Kikundi kwa sasa kinasimamiwa na viongozi wafuatao:-

JINA WASIFU

Edson Justine  Rwambogo

Ndugu Edson Justine Rwambogo alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2015. Kabla ya kuwa Mwenyekiti wa kikundi, Edson alishika nafasi ya udhibiti huku akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa kikundi (2021-2022) na baadae kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kikundi Mwaka 2022 nafasi anayoishikilia mpaka sasa.

 

Ndugu Edson ana uzoefu wa miaka 8 katika fani ya Tathmini na ufuatiliaji (M&E) kupitia miradi ya vikundi, Kilimo na Afya, amefanya kazi katika idara ya maendeleo kwenye miradi mbalimbali ndani ya kanisa la AICT Tanzania na AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe (Mratibu wa miradi Wilaya ya Ukerewe na Bunda.

 

Kwa  sasa ameajiriwa na kanisa la AICT MUD kupitia mradi wa Kilimo Hifadhi ni msimamizi wa mradi huo wilaya ya Bunda.

 

Edson ni muhitimu wa chuo cha Tumaini University Dar Es Salaam Collage katika fani ya Mawasiliano ya Umma ngazi ya Shahada (Mass Communication) sasa ni mwanafunzi wa Chuo cha Open University anachukua masomo ya Shahada ya Uzamili (Masters in Community Economic Development (MCED).

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati Tendaji: Mwenyekiti

Sekretarieti ya Uongozi: Mwenyekiti

John Stauffer Warioba

John Stauffer Warioba

 

Ndugu John, ni miongoni mwa waanzilishi wa kikundi hiki cha WYT. Amekuwa Katibu wa kikundi hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2015 hadi mwaka 2019 kabla ya kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa CELL ya Waebrania (2020). Kwenye Mkutano mkuu wa mwaka 2021 ndugu John alichaguliwa kwa mara nyingine kushika wadhifa wa katibu wa kikundi kwa miaka mingine miwili kwa mujibu wa katiba ya WYT.

 

Ndugu John ana uzoefu wa kufanya kazi za Miradi/ maendeleo ya jamii kwa zaidi ya miaka 10. Pia amekuwa mkufunzi na msimamizi wa vikundi vya kuweka na kukopa vinavyotumia mifumo mbalimbali kama vile PAMOJA, SELF HELP GROUP, VICCOBA na WORTH kwa zaidi ya miaka 9.

 

Kwasasa ndugu John anafanya kazi na kanisa la AICT MUD, idara ya maendeleo kama Afisa Miradi mwandamizi.

 

John ni mhitimu wa Chuo kikuu cha Dodoma katika fani ya Utawala wa Biashara (BBA).

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati Tendaji: Katibu

Sekretarieti ya Uongozi: Katibu 

 

Murungi Kajumulo

 

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati Tendaji: Katibu Msaidizi

Sekretarieti ya Uongozi: Katibu Msaidizi

 

 

 

Benjamin Mosha

Benjamin Mosha

 

Ndugu Benjamini Mosha alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2019 na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CELL ya Wasamaria (2020).

Ndugu Benjamin ana uzoefu wa zaidi ya miaka 3 katika fani ya Uhasibu. Kwasasa Mosha anafanya kazi na kanisa la AICT MUD kama Mhasibu Msaidizi katika idara ya Utawala na Fedha.

Charles Loleku ni mhitimu wa fani ya Uhasibu na Fedha kutoka chuo kikuu cha Ushirika (MOCU)

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati Tendaji: Mhazini

Sekretarieti ya Uongozi: Mhazini

 

 

 

 Emmanuel Bhoke

 

Ndugu Emmanuel Bhoke amekuwa mwenyekiti wa Kikundi cha WYT tangu mwaka 2018. Kabla ya hapo alikuwa ni mmoja wa viongozi wa bodi ya Mikopo katika SACCOS ya Nyasho. Pia anauzoefu wa kufanya kazi za maendeleo ya jamii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwasasa anafanya kazi na kanisa la AICT MUD, Idara ya Maendeleo kama Dereva na Mwinjilisti.

 

 

 

 

 Marko Maseko

Rev. Marko Maseko

 

Mchungaji Marko Maseko alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2015 na alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CELL ya Ebeneza mwaka 2018 nafasi anayoishikilia mpaka sasa.

Pamoja na kuwa mwenyekiti wa CELL, Maseko ni Mchungaji wa kanisa la AICT Kiabakari na Mratibu wa idara ya Elimu ya Kikristo-AICT MUD.

Pamoja na kufanya huduma za kichungaji kwa miaka 6 ndugu Maseko pia anauzoefu wa kufanya shughuli za maendeleo ya jamii kama mkulima mkufunzi kwenye mradi wa kilimo Hifadhi unaotekelezwa na AICT MUD.

Ndugu Marko Maseko ni mhitimu wa Chuo cha Biblia Majahida katika fani ya theolojia.

 

 

Mwipagi Magawa

Mwipagi Magawa

 

Ndugu Mwipagi Magawa alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2019 na kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi (2020).

Ndugu Mwipagi ana uzoefu wa zaidi ya miaka 6 katika fani ya Uhasibu. Mwipagi amewahi kufanya kazi na taasisi mbalimbali kama vile CRDB Moshi, AICT HQ-Mwanza na sasa anafanya kazi na kanisa la AICT MUD kama Mhasibu Msaidizi katika idara ya Utawala na Fedha.

Mwipagi ni mhitimu wa fani ya Uhasibu, Ushirika pamoja na fedha kutoka chuo kikuu cha Ushirika (MOCU)

 Felix Assey

Felix Assey

 

Ndugu Felix Assey alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2017 na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CELL ya Yerusalem mwaka 2018.

Felix Assey ni mtaalam wa Kilimo na Ufugaji na ameajiriwa na kanisa la AICT MUD kama Meneja wa Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Mseto (Agroforestry Taining Center-ATC) kilichopo Bweri Musoma.

Ndugu Assey anauzoefu wa zaidi ya miaka 13 katika kusimamia miradi ya Kilimo na ufugaji.

Assey ni Mhitimu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo jijini Arusha katika fani ya Misitu.

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Cell ya Kikundi: Mwenyekiti wa CELL ya Yerusalemu

 

 

 

Salome Machele

 

 

Joyce Shabani William

 

 

Paul Dotto Kasheto

 

 

 Justine Jumanne

Justine Jumanne

 

 

Ndugu Justine Jumanne alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2015 kama mwanachama mwanzilishi. Justine amekua mjumbe wa secretariet ya WYT toka mwaka 2016 hadi sasa, mwaka 2017 alichaguliwa kuwa   Mwenyekiti wa CELL ya Wasamaria kabla ya kuchaguliwa kupitia mkutano mkuu wa mwaka 2019 kuwa Mdhibiti wa Kikundi.

Kwasasa Justine anafanya kazi na kanisa la AICT MUD kama afisa uwanda kwenye idara ya Maendeleo. Justine anauzoefu wa kusimamia na kuendesha shughuli za vikundi vya kilimo, vikundi vya kuweka na kukopa na utoaji wa elimu ya uhifadhi mazingira na upandaji miti kwa zaidi ya miaka 5. 

Ndugu Justine ni muhitimu wa chuo cha Maendeleo ya jamii Buhare katika fani ya maendeleo ya jamii (Community Development-CD). Kwasasa ndugu Justine shahada ya Maendeleo na Mipango katika chuo kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania)

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati ya Uchumi na Uwekezaji: Mwenyekiti

 Emmanuel Saitoti  

Ndugu Emmanuel Saitoti alijiunga na kikundi cha WYT mwaka 2015. Kabla ya kuwa Mhasibu wa kikundi, Saitoti alishika nafasi ya udhibiti kwa miaka mitatu (2015-2017) na baadae kuchaguliwa kuwa Mhasibu wa kikundi mwaka 2018 nafasi anayoishikilia mpaka sasa.

Ndugu Saitoti ana uzoefu wa miaka 7 katika fani ya uhasibu, huku akifanya kazi katika vitengo na idara mbalimbali ndani ya kanisa la AICT (Mhasibu idara ya Afya, Mhasibu Idara ya Utawala na Fedha, Mhasibu wa Mradi wa Compassion) na kwa sasa ameajiriwa na kanisa la AICT MUD kupitia mradi wa Compassion International kama Mkurugenzi wa kituo cha Watoto-Nyasho.

Saitoti ni mhitimu wa chuo cha uhasibu - Tanzania Institute of Accountancy (TIA) katika fani ya Uhasibu (Accounting) na kwasasa ni mwanafunzi wa masomo ya CPA.

 

Nafasi za Uongozi katika Kikundi

Kamati ya Uchumi na Uwekezaji: Katibu