sw Swahili en English

Wadau wa WYT

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Ijumaa, 14 Mwezi wa 2, 2020 19:20
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 624

Taasisi za kifedha: NMB Bank & CRDB Bank

Taasisi za kifedha zinazoshirikiana na kikundi katika kutoa huduma za kifedha ni NMB na CRDB Bank.

Serikali (Manispaa ya Musoma)

Halmashauri ya Musoma imekuwa mdau mkubwa kwa kikundi chetu hasa idara ya Maendeleo katika kutoa elimu, ushauri na kutuunganisha na fursa mbalimbali zinazohusu vikundi vya kijamii.

BizXpert, Inc.

Hii ni kampuni ya kutengeneza Mifumo ya Kielektroniki (Computer Softwares) yenye makao yake makuu Budapest, Hungary. BizXpert, Inc. ilitoa kibali cha kutumia mfumo wa elektroniki wa Biz-Expert ambayo kikundi kinatumia kwa kutunza kumbukumbu zake za msingi hii ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu za malipo yote ya kikundi na kutuma hati za Madai na risiti kwa wanakikundi.

Alliance Life Assurance Ltd

Hii ni kampuni ya Bima ya Mikopo inayofanya kazi ikishirikiana na benki ya CRDB kupitia CRDB Insurance Brokers kutoa huduma za Bima mbalimbali. Kikundi kilijiunga na huduma ya Bima ya Mikopo mwaka 2018 kupitia CRDB Insurance Brockers ambaye ni mshirika mwenza wa Alliance Life Assurance Ltd kwa ajili ya kukatia bima mikopo yote inayotolewa na kikundi.

AICT MUD

Kanisa AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe ni mdau muhimu ambaye kwa sehemu kubwa alifanikisha kuwepo kwa kikundi hiki kwani ni mwajiri aliyekutanisha wanakikundi wengi waliojiunga na kikundi hiki ambao walipata uzoefu wa kufanya kazi za vikundi na kuja na wazo la kuwa na kikundi hiki kwani wengi wao wameajiriwa au waliwahi kuajiriwa na AICT MUD.

Microsafi.

Hii ni kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ambayo kikundi kimekuwa kikishirikiana nayo katika kutoa huduma ya tovuti/wavuti ikiwa ni pamoja na ushauri na matengenezo. Kupitia huyu mdau kikundi kimeweza kujitangaza ndani na nje ya nchi.