sw Swahili en English

Maombi na Vikao, na Edson Rwambogo

  • Kundi: Elimu
  • Imechapwa Juma nne, 31 Mwezi wa 5, 2022 14:00
  • Imendikwa na admin
  • Vibofyo: 683

MSINGI IMARA WA UONGOZI KATIKA TAASISI

Na Rwambogo Edson.

Katika uongozi kuna baadhi ya mambo muhimu ya kuyazingatia bila kujali uwezo na uzoefu wa taasisi au kiongozi. Mambo mawili yanatosha kuimarisha taasisi yako, jambo la kwanza ni Maombi na jambo la pili ni Vikao.

Maombi. Hapa namaanisha ibada, ibada katika taasisi ni sehemu muhimu sana katika kujenga taasisi yenye mwelekeo mmoja katika imani. Hata kama taasisi imeajiri watu wa imani tofauti lakini lazima imani hizo msingi wake ni Mungu kupitia imani tofauti. Hivyo ni muhimu sana kwa kila taasisi kuwe na kipindi cha ibada eidha ibada ya kuombea shughuli au ibada kwa kushirikiana neno la siku (Morning Devotion) kabla ya kuanza majukumu.

Katika ofisi nyingi zisizokua na imani yoyote au zisizojipa muda wa tafakari ya neno la Mungu kuna maumivu makali sana mioyoni mwa watumishi. Wapo waliodhulumiana fedha majeraha yao hayajaponywa na wadhulumaji hawajawahi kupata kutafakari wakiwa wanawaona waliowatendea ubaya huo.

 

Lakini mnapo kua na utamaduni wa kupeana neno hasa kwa utaratibu wa kila mtumishi kupata nafasi ya kuhubiri au kuongoza maombi ya taasisi hapo walio na kinyongo hufunguka. Ibada ya pamoja inasaidia kuleta umoja katika ulimwengu wa roho  kwa kuwaunganisha watu hata kama hawataombana msamaha kuna kitu kinajengeka moyoni mwao (upendo, huruma, undugu na amani). 

Vikao. Hapa ni mahali muhimu sana kwa viongozi na wanaoongozwa kufahamiana, kusikilizana lakini pia kupeana mtazamo wa kitaasisi. Mahali hapa watumishi na watumisha hawapaswi kuja na maamuzi yao bali waje na mapendekezo ili kutoa mwanya na milango ya majadiliano katika kujenga taasisi imara zenye mwelekeo wa pamoja.

Kuna faida nyingi za vikao;  nitajaribu kuelezea faida hizi tatu.

  • Kuleta mawazo jumuishi ili watu wamiliki tasisi.Miongoni mwa mambo ambayo binadamu hana masihara nayo katika utu wake ni suala la kusikilizwa. Binadamu yeyote anaamini ana maoni na mawazo bora kuliko binadamu yeyote. Wazo la binadamu hupingwa na kubadilishwa mwelekeo kwa kujibiwa na siyo kupuuzwa, vikao ni sehemu pekee ambayo inaweza kumjengea mtu uwezo wa kujenga hoja na kuitetea na ikishindikana nafsi inapunguza hasira na kukubaliana na mawazo ya wengi. Pamoja na masuala mengine yote kupitia vikao inasaidia watumishi kuheshimu na kumiliki maamuzi yao kwa kuwa wao huwa sehemu ya kuanzisha wazo lililopitishwa.

 

  • Ni mahali pa kupumua na kutema nyongo. Binadamu hujisikia salama kueleza shida zao, uonevu waliofanyiwa na mateso yao mbele za watu wengi kuliko njia za vificho. Waongozwa na waongoza hutamani wanayotendewa sirini yaonekane hadharani lakini nafasi ikikosekana huchukua hatua ya kususa na kutelekeza imani yao kwa viongozi wao. Watawala hupokea kero nyingi nzito katika mikutano ya hadhara kuliko wanapowahimiza watu waende ofisini kwao kutoa malalamiko yao.

  • Kujenga umoja na mshikamao. Hakuna njia ya mkato katika kuwaleta watu Pamoja nje ya vikao na majadiliano. Taasisi zinatakiwa kuwaleta watu wake Pamoja kupitia vikao vinavyojulikana agenda zake ikiwezekana watu waombwe kupendekeza agenda za vikao hivyo. Kupitia njia za vikao masikilizano kupitia kushindanisha hoja zenye nguvu na dhaifu huwafanya watu kujiona wamoja na kujenga moyo waushindani wa wazi.

 

Kwa Mawasiliano:

Namba ya Simu: 0765 355 105

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.