sw Swahili en English

Kuhusu Walk Your Talk Group

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Juma tano, 05 Mwezi wa 2, 2020 10:30
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 2562

WYT ni kikundi cha kijamii (SHGs) kilichoanzishwa na wafanyakazi wa kanisa la AICT MUD, idara ya maendeleo mwaka 2015. Kikundi cha WYT kinatambuliwa na serikali kwa kupitia usajili uliofanyika katika ofisi za Manispaa ya Musoma tarehe 27/05/2015 kwa utambulisho wa barua yenye kumbukumbu namba “Kumb Na. HMM/UT/VK/418”. Ofisi ya kikundi hiki kinapatikana katika jengo la ofisi kuu la kanisa la AICT MUD iliyopo Bweri, Musoma.

Kikundi hiki kiliundwa kwa lengo kuu la kushughulikia masuala ya kijamii na kiuchumi ya wanakikundi na jamii kwa ujumla. Kikundi hiki pamoja na shughuli/huduma zingine kinafanya kazi za kuweka na kukopa (Saving and Credits) kupitia mfumo wao waliouandaa wenyewe kwa kutumia uzoefu waliyopata katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa ikihamasisha uundaji wa vikundi vya kuweka na kukopa kwa kutumia mifumo mbalimbali kama vile VICCOBA, SILK, WORTH, SELF HELP GROUPS na PAMOJA.

Kikundi cha WYT ni kikundi kinachozingatia suala la usawa katika kutoa haki na huduma. Kikundi hiki hakibagui jinsi, elimu, kabila wala rangi ya mtu katika usajili wa wanakikundi. Kwasasa kikundi hiki kina jumla ya wanachama 30, hii ikiwa ndio ukomo wa idadi ya wanachama kikatiba. Kwenye idadi hii, wanawake ni 11 sawa na asilimia 37% ya wanachama wote. Idadi hii imekuwa kutoka wanawake 3 kwa mwaka 2015.