sw Swahili en English

Mfumo wa Utawala na Uongozi wa Kikundi

  • Kundi: Fahamu
  • Imechapwa Alhamisi, 27 Mwezi wa 2, 2020 09:16
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 1968

Mfumo wa uongozi katika kikundi cha WYT umegawanyika katika maeneo makuu 3; Mfumo wa kwanza ni Kamati tendaji (KT), Mfumo wa Pili ni Sekretarieti ya Uongozi (SU) na Mfumo wa Tatu ni CELL za Kikundi (CK). Msemaji mkuu wa kikundi ni Mwenyekiti wa Kikundi.

Shughuli za siku kwa siku za kikundi zinafanywa na kamati tendaji; Sekretarieti ya Uongozi inashughulika na masuala ya mipango na usimamizi wa mikopo ya kikundi. Pia inahusika katika kupanga na kusimamia masuala yote yanayohusu uwekezaji katika kikundi. CELL za kikundi ni ngazi ya chini ya mfumo wa uongozi wa kikundi cha WYT lakini chenye maamuzi ya kusajili wanakikundi pamoja na kupitisha na kusimamia mikopo ya wanakikundi katika ngazi ya CELL.

Pamoja na mifumo ya uongozi katika kikundi hiki cha WYT, Mkutano mkuu wa wanakikundi wote (AGM) ndicho chombo chenye maamuzi ya mwisho juu ya mambo yote ya kikundi na mipango yote ya kikundi inapitishwa na Mkutano mkuu wa kikundi unaofanyika mara moja kwa mwaka.