sw Swahili en English

Mkutano wa Kikundi kwa njia ya Mtandao

  • Kundi: Taarifa
  • Imechapwa Juma pili, 29 Mwezi wa 5, 2022 19:13
  • Imendikwa na admin
  • Vibofyo: 299

Kikundi cha WYT kimefanikiwa kwa mara nyingine kufanya Mkutano wake wa Robo ya Kwanza ya Mwaka 2022 kwa njia ya Mtandao  kwa ufanisi mkubwa  mnamo tarehe 23/04/2022. Huu umekuwa ni mkutano wa tatu wa kikundi uliofanyika kwa njia ya mtandao tangu kikundi hiki kilipoanza mchakato wa kuboresha mifumo yake ya upashanaji wa habari na taarifa kwa njia ya mitandao (Zoom meetings). Mkutano huu ulihudhuriwa na wanachama 25 kati ya wanachama wote 30 wa kikundi cha WYT.

Mikutano ya mitandao imekuwa ni njia nzuri ya kuhakikisha kila mwanakikundi anakuwa sehemu ya mijadala inayoendelea kwenye kikundi hasa kwa wale wanaoishi nje ya kanda ya ziwa kwani wameshiriki ipasavyo katika kutoa maoni na michango yao. Mikutano kwa njia ya mitandao si tu kwamba inatoa fursa ya kila mwanakikundi kushiriki katika mijadala ya kikundi lakini pia inapunguza gharama za usafiri  na gharama zingine za kujikimu kwa wanakikundi wanaotoka nje ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara. 

Napenda kuwashukuru wanakikundi wote na wadau wetu kwa michango na mawazo yao yanayofanya kikundi hiki kiwe kikundi cha tofauti na vikundi vingine ndani na nje ya nchi kwa  namna kinavyoendeshwa na kutilia mkazo suala la utaalamu na uweledi katika kuendesha shughuli za kikundi.

Imetolewa na :

Ofisi ya Katibu wa Kikundi,

Walk Your Talk (WYT)