sw Swahili en English

Ufadhili wa Kozi fupi kwa Wanakikundi

  • Kundi: Taarifa
  • Imechapwa Alhamisi, 13 Mwezi wa 2, 2020 04:22
  • Imendikwa na Super User
  • Vibofyo: 330

Ninapenda kuwajulisha kwamba Kikundi chetu cha  Walk Your Talk katika Mpango Mkakati wa Kikundi wa Miaka 5 (2020/2025)katika  Eneo la Pili la Kimkakati ambalo ni Ustawi wa uendeshaji wa kikundi kiuongozi na kiutawala; mojawapo ya malengo ni kuwaendeleza wanakikundi katika fani mbalimbali(kozi fupi za mafunzo) ili kuongeza ujuzi.

Katika kutekeleza lengo hilo kwa Mwaka 2020/21 Mkutano Mkuu wa kikundi uliofanyika tarehe 12/1/2020 uliidhinisha kiasi cha Tsh.700,0000/= kwa ajili ya kuwasomesha wanakikundi katika kozi mbalimbali.

Hivyo basi uongozi wa Kikundi cha WYT unakaribisha maombi kutoka kwa wanakikundi wenye kuhitaji ufadhili katika kozi ambazo wangependa kusoma.Katika maombi hayo watachaguliwa wanakikikundi 2 ambao watafadhiliwa katika masomo hayo.

MASHARTI KWA WAOMBAJI WOTE.

  1. Iandikwe barua ya maombi kwa Katibu wa Kikundi kupitia kwa Mwenyekiti wa Cell kuonesha
  • Aina ya kozi
  • Chuo
  • Muda wa Masomo
  • Gharama halisi za Kozi.
  1. Kikundi kitagharamia si zaidi ya Tsh.350,000/=(Kama itakuwa zaidi gharama nyingine zitatoka kwa mwanakikundi husika)
  2. Mwombaji awe tayari gharama hizi kulipwa moja kwa moja Chuoni au mtoa mafunzo.
  3. Mwombaji awe tayari kutoa maendeleo yake kila mara atakapotakiwa kufanya hivyo na Viongozi au kikundi cha WYT au uongozi kupata maelezo kutoka chuo husika /wakufunzi kuhusu maendeleo ya mwanakikundi.
  4. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 March 2020.

Imetolewa na

Davis Rweyemamu Dominick

Katibu WYT

12.02.2020