sw Swahili en English

TAARIFA MUHIMU KWA WANAKIKUNDI WOTE KUHUSU MLIPUKO WA UGONJWA WA CORONA(COVID-19) NCHINI.

  • Kundi: Taarifa
  • Imechapwa Juma nne, 31 Mwezi wa 3, 2020 10:05
  • Imendikwa na admin
  • Vibofyo: 422

Wapendwa Wanakikundi wa WYT, Bwana Yesu Asifiwe;

Kama tunavyofahamu kwamba dunia sasa imekumbwa na Ugonjwa wa CORONA(COVID- 19) ambao umesambaa hadi kufika nchini kwetu na tayari serikali imethibitisha wagonjwa kadhaa na kutoa tamko juu ya kuchukua  tahadhari ili kuhakikisha tunajilinda na kuwalinda wale wanaotuzunguka.

Kwa kuwa hili  ni tukio la kidunia nasi wana Walk Your Talk hakuna namna tunaweza kujiepusha kuwa sehemu ya mapambano , kujikinga na kuhakikisha kwamba tunakuwa katika mazingira salama na kuilinda jamii inayotuzunguka dhidi ya maambukizi.

Kwa kulitambua hilo Sekretariet ya Uongozi(SU) –WYT katika kikao kilichofanyika tarehe 28 Machi 2020 mojawapo ya agenda ilikuwa ni kujadili kuhusu athari zinazoweza kujitokeza  kiafya na kiuchumi hivyo kuathiri mwenendo wa kikundi. Pamoja na kujadili Sekretariet ya uongozi inapenda kuwajulisha wanakikundi wote kwamba;

  1. Mkutano wa Kikundi wa Robo ya Kwanza uliopangwa kufanyika tarehe 18 April 2020 umeahirishwa ili kufuata utaratibu wa serikali wa kuepuka mikusanyiko na hii itatuweka katika mazingira salama ya kuepuka maambukizi.Taarifa ambayo ilipaswa kusomwa katika mkutano huo itatumwa kwa wanakikundi kupitia barua pepe na kama kutakuwa na jambo la muhimu la kujadili litajadiliwa kupitia mitandao katika kundi la whatsapp la WYT. Tarehe mpya ya mkutano itatangazwa kama hali itaimarika na serikali kuruhusu mikusanyiko.
  2. Pamoja na kwamba kutakuwa na athari kiuchumi na huenda zimeanza kujitokeza Sekretariet ya Uongozi imeazimia kwamba ununuzi wa hisa za Kawaida, Mkupuo, Marejesho ya Mikopo na michango mingine itaendelea kama ilivyopangwa hadi hapo baadaye itakavyoamriwa vinginevyo kulingana na hali halisi ya uchumi na athari za ugonjwa kwa dunia na nchi yetu.
  3. Sekretariet ya Uongozi inawashauri wanakikundi wote kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na wataalam namna ya kujikinga na maambukizi ya Corona.Aidha mnashauriwa katika kipindi hiki kutumia njia mbadala za kulipia michango mbalimbali zinazoepusha mikusanyiko kama M-Pesa, tiGo Pesa, Airtel Money , Hallotel Money na Internent Banking ili kuhakikisha tunakuwa salama wakati wote.
  4. Pamoja na kuchukua tahadhari hizo, kwa kuwa Msingi wetu ni kumtegemea Mungu tuzidi kuomba Mungu atuepushe na gonjwa hili hatari kwani msaada wetu unatoka kwake.

Niwatakie baraka za Bwana.

IMETOLEWA NA:

Davis Rweyemamu Dominick

Katibu wa Kikundi

Tarehe : 30 Machi 2020.