Toleo hili la Katiba ya Walk Your Talk Group ni Toleo la tatu tangu kuanzishwa kwa kikundi hiki tarehe 20/12/2014 baada ya Maboresho ya Katiba ya Toleo la Pili iliyokuwa ikitumika tangu mwaka 2016. Maboresho haya yamefanyika kutokana na mapungufu yaliyoonekana kwenye katiba ya toleo la pili ya kikundi ya mwaka 2016.
Uandaaji wa mpango mkakati huu ulitokana na utekelezaji wa mipango ya mwaka mmoja mmoja wa kikundi hiki cha WYT. Kwa vile kikundi hiki hakikuwa na mpango mkakati kwa takribani miaka 5 ya uendeshaji wa shughuli zake, wanakikundi kupitia mikutano ya vikundi waliona ni vyema kikundi kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano ili kikundi kiweze kuwa na maono ya muda mrefu yanayoweza kupimika.
WYT ni kikundi cha kijamii (SHGs) kilichuondwa na wafanyakazi wa kanisa la AICT MUD, idara ya maendeleo mwaka 2015. Kikundi cha WYT kinatambuliwa na serikali kwa kupitia usajili uliofanyika katika ofisi za Manispaa ya Musoma tarehe 27/05/2015 kwa utambulisho wa barua yenye kumbukumbu namba “Kumb Na. HMM/UT/VK/418”. Ofisi ya kikundi hiki kinapatikana katika jengo la ofisi kuu la kanisa la AICT MUD iliyopo Bweri, Musoma.
Hii ni Taarifa inayoonesha maendeleo ya kikundi katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 (Januari-March 2022) kulingana na mpango mkakati wa kikundi wa Miaka 5. Ili kupata maelezo zaidi unaweza kuipakua kwa kubofya kitufe cha Download kilichopo upande wa kulia ili uweze kujifunza zaidi kile tunachofanya kama kikundi. Tunakaribisha wadau mbalimbali tunaoweza kushirikiana nao katika kufikia malengo ya kikundi.
Sheria, Kanuni na Taratibu za Kikundi cha Walk Your Talk (WYT)