sw Swahili en English

Ujumbe Kutoka kwa Mwenyekiti

 Nawasalimu wote kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo!!.

Kikundi chetu kinaendelea kukua na kustawi, huu ni mchango wa kila mmoja wetu katika kukiendeleza kikundi chetu kupitia maombi, michango, mikopo na mali zetu ili kufikia malengo yetu tuliyojiwekea.

Sisi kama viongozi wa kikundi tunawajibu wa kusimamia yale mnayo tutaka kuyafanya. Kwa maneno hayo niwaombe ndugu zangu wana WYT kusoma na kupitia miongozo ya kikundi zikiwemo sheria na kanuni mara kwa mara kujikumbusha lakini pia kuweka mikakati binafsi katika utekelezaji.

Uongozi tumejipanga kusimamia mambo matano kwa ufanisi zaidi

  1. Kuhakikisha usalama wa fedha na mali za kikundi
  2. Kusimamia sheria na kanuni tulizojiwekea
  3. Kuusimamia mpango mkakati wetu wa miaka mitano kama ipasavyo
  4. Utoaji wa mikopo kwa wakati na kwa ukamilifu
  5. Kuendelea kuhamasisha utoaji wa michango kwa wakati na kufanya marejesho kwa mujibu wa kanuni na sheria zetu.

Kwa hayo nawatakia utafutaji mwema na uwekezaji mwema wana WYT wenzetu, tuendelee kupendana na kusaidiana pale mwenzetu anapokwama, kwa sehemu kubwa majukumu mengi na makubwa yapo mabegani mwetu hatuna Mjomba wakulinda tunu za WYT.

Ahsanteni

 

Edson Rwambogo

Dira Yetu (Vision)

Kikundi cha kijamii kinachoongoza nchini kwa kuchochea kikamilifu ustawi wa maendeleo ya wanakikundi na jamii

Dhamira Yetu (Mission)

Kuwa kikundi cha kijamii kinachoendeshwa kitaalamu kwa kuzingatia na kukuza ustawi wa wanakikundi, familia zao na jamii kwa kuwajengea mifumo imara ili kujitegemea kiuchumi, kiroho na kijamii

Taarifa za Karibuni

More in Taarifa  
Idadi ya Miradi
Idadi ya Wanachama
Idadi ya Huduma
Idadi ya Wadau

Ramani ya Tanzania na Mikoa wanayoishi wanakikundi

Maeneo wanayotoka wanakikundi wa WYT

Wanakikundi wa WYT wanatoka katika mikoa mbalimbali katika nchi yetu ya Tanzania. Kwetu sisi umbali anaotoka mwanachama si tatizo kutokana na mifumo  imara ya uendeshwaji wa kikundi iliyowekwa pamoja na matumizi ya TEHAMA. Kwasasa tuna wanachama katika mikoa ya Mara (23), Mwanza (3), Dodoma (1), Mbeya (1), Simiyu (1) na Shinyanga (1).

Yaliyojiri Hivi Karibuni

Msaada kwa jamii
400
...
By Super User | In Matukio

Msaada kwa jamii

Read more
Mkutano wa wadau
309
...
By Super User | In Matukio

Mkutano wa wadau

Read more
Washiriki wetu
1272
...
By Super User | In Matukio

Washiriki wetu

Read more
Bishop
586
...
By Super User | In Matukio

Bishop

Moja ya nyakati za furaha kwa baadhi ya wanakikundi kumtembelea aliyekuwa...

Read more
Mwanakikundi Justine Jumanne akifurahia...
360
...
By admin | In Matukio

Mwanakikundi Justine Jumanne akifurahia...

Read more
Ziara ya Mapumziko ya wanakikundi...
394
...
By admin | In Matukio

Ziara ya Mapumziko ya wanakikundi...

Read more
Baadhi ya Wanakikundi wa WYT baada...
381
...
By admin | In Matukio

Baadhi ya Wanakikundi wa WYT baada...

Read more
TANZIA
14
...
By Super User | In Matukio

TANZIA

Read more

Walk Your Talk Group

Lengo kuu la kuanzishwa kwa kikundi hiki lilikuwa ni kuwasaidia wanakikundi kuboresha Maisha yao kupitia kuanzisha mfumo wa kununua Hisa na kukopeshana na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya kijamii. soma zaidi...

Mawasiliano

Musoma, Mara
P.O.BOX: 605,
+255 747 599 825
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

 

Jisajili Kupata Taarifa